Idadi ya waliofariki yaongezeka Yemen

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanajeshi aliyejeruihiwa katika shambulio mjini Sanaa

Takriban wanajeshi 90 wameuwawa katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Zaidi ya wengine 300 walijeruhiwa katika mlipuko huo uliotokea karibu na ikulu ya rais wakati wanajeshi walipokuwa wakijiandaa kwa gwaride la kijeshi.

Ripoti zinaarifu kuwa mshambuliaji wa kujitoa mhanga naye alikuwa amevalia magwanda ya jeshi.

Duru kutoka kwa kundi la kigaidi la Al-Qaeda zinasema kuwa kundi hilo ndilo lilihusika na shambulizi hilo.

Jeshi la Yemeni hivi sasa linaendesha harakati za kijeshi dhidi ya kundi hilo kusini mwa nchi.

Hili ndio shambulio kubwa ziaid kutokea mjini Sanaa tangu rais Abd-Rabbuh Mansour kuchukua mamlaka mwezi Februari.

Mwanajeshi mmoja alielezea alichoshuhudia akisema kuwa waliohusika lazima wachukuliwe hatua, wito ambao pia ulitolewa na maafisa kadhaa wa jeshi.