Ukiukwaji wa haki za binadamu S.Lanka

Image caption Sarath Fonseka

Mkuu wa zamani wa jeshi la Sri-lanka Sarath Fonseka aliyeachiliwa kutoka gerezani hiyo jumatatu ameishauri nchi yake kushirikiana na wachunguzi wa kimataifa wanaochunguza madai ya uhalifu wa kivita nchini humo.

Bwana Fonseka aliiambia BBC kuwa mienendo ya viongozi wa serikali inaashiria kuwa wanaficha mambo fulani kuhusiana na madai hayo ya uhalifu wa kivita.

Generali huyo wa zamani amesema hahofii kujibu maswali yoyote.

Bwana Fonseka aliongoza jeshi la Sri lanka kuangamiza waasi wa Tamil tigers mwaka 2009 lakini baadaye akakososana na rais Mahinda Rajapakse.