Mpango wa dharura dhidi ya Polio

Haki miliki ya picha
Image caption Chanjo dhidi ya Polio

Shirika la Afya la umoja wa Mataifa (WHO) linatazamia kutangaza maradhi ya kupooza, polio kama maradhi yanayopaswa kushughulikiwa kwa dharura.

Hii ni baada ya mlipuko wake kugunduliwa Barani Ulaya, Afrika na Asia.

Polio inapatikana kwa wingi wakati huu katika Afghanistan, Pakistan na Nigeria na kumetokea maambukizi mapya zaidi katika mataifa ambayo awali yalikuwa yametangazwa kuwa maradhi hayo yameangamizwa.

Mwandishi wa BBC ameeleza kuwa vita na ukosefu wa imani katika chanjo katika mataifa fulani; inamaanisha kuwa watoto katika mataifa fulani hayapati kinga inayofaa.

Afisaa mmoja wa WHO alisema kwamba iwapo juhudi za kimataifa za kuangamiza polio hazitafaulu, maradhi hayo yataongezeka na kuwa mengi zaidi duniani.