ANC kimeitaka mahakama iondowe mchoro

Sehemu za siri zazibwa Haki miliki ya picha AP
Image caption Sehemu za siri zazibwa

Mawakili wanaomwakilisha Rais wa Afrika ya kusini, Jacob Zuma, wameitaka mahakama ione kwamba mchoro unaoonyesha sehemu zake za siri unaondolewa hadharani. Mchoro huo uliharibiwa mnamo siku ya jumanne na waandamanaji wawili walioumwagia rangi.

Kufuatia jaribio hilo la kuuharibu mchoro, chumba cha maonyesho ulipokua kimefungwa.

Chama cha ANC kimeutaja kama ufidhuli, kukosa adabu na Bw.Zuma na chama chake wanataka nakala zote ziondolewe kwenye mtandao na kwingine ziliko.

Mwandishi wa BBC Milton Nkosi aliyehudhuria kikao cha mahakama hio mjini Johannesburg amesema kua ilibidi Majaji waahirishe kesi hio baada ya wakili wa Bw.Zuma, Gcina Malindi kuangua kiliyo wakati akizungumza kuhusu juhudi za kupinga ubaguzi wa rangi.

Chama cha ANC kinachukua hatua dhidi ya chumba cha maonysehjo ya picha pamoja na wavuti ijulikanayo kama City Press.

Image caption Rais Zuma na miondoko ya kwao

Kesi hii imeonekana kama chaguo baina ya uhuru wa kujieleza na haki ya hadhi ya mtu yote ambayo yanalindwa na sheria za Afrika ya kusini..

Mchoro huo ulipewa jina The Spear, ama mkuki, unakadiriwa kugharimu dola za Marekani $14,000 ulichorwa na Brett Murray, mchoraji maarufu kwa misimamo yake ya kisiasa na kazi yenye utatanishi, na umeisha uzwa.

Mamiya ya wafuasi wa chama cha ANC walikusanyika nje ya mahakama. Msemaji wa chama hicho Jackson Mthembu Temba aliliambia shirika moja la habari SAP kua raia wengi watajitokeza kulinda hadhi na heshima ya ANC na kiongozi wake Jacob Zuma.