Mauaji makubwa yatokea Houla, Syria

Wanaharakati wa upinzani nchini Syria wameutaka Umoja wa Mataifa na wachunguzi wake kuchukua hatua zaidi kuwalinda raia baada ya kile wanachokitaja kuwa ni mauaji makubwa katika mji wa Houla, kwenye eneo la Homs.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Wanasema watu kama 90 waliuliwa na majeshi ya serikali Ijumaa.

Picha isiyothibitishwa kutoka mji huo, inaonyesha watoto wengi kati ya waliokufa.

Wanaharakati hao wametaka maombolezo ya kitaifa ya siku moja yafanyike.

Mwandishi wa BBC katika eneo hilo amesema, iwapo habari hizo zitathibitishwa, basi hiyo itakuwa siku ya umwagaji damu mkubwa kabisa, tangu makubaliano ya kusitisha mapigano kuanza majuma sita yaliyopita.