Wapiganaji wa Mali waungana

Milio ya risasi ya sherehe ilisikika katika miji ya kaskazini mwa Mali, pamoja na Timbuktu, baada ya makundi ya wapiganaji wanaoshindana, kutangaza kuwa wameungana ili kuunda taifa la Kiislamu.

Haki miliki ya picha AFP

Msemaji wa kundi la Waislamu la Ansar Dine, alieleza kuwa watafanya kazi pamoja na kundi la Wa-Tuareg la vuguvugu la ukombozi wa Azawad.

Waandishi wa habari wanasema uamuzi wa Ansar Dine kubadilisha sera yake na sasa kutaka kujitenga na kusini, ni pigo kubwa kwa viongozi katika mji mkuu wa Mali, Bamako.

Wapiganaji wamezidi kudhibiti eneo la kaskazini la Mali mwezi wa March, baada ya mapinduzi.