Wa Sudan wasusia chakula kizuizini

Watu hao ni kutoka mikoa mitatu ya Darfur na miongni mwao ni kutoka makabila ya Zaghawa, Tama, Mirra,Berti na Tunjur. Tayari imethibitika kua mmoja kati yao aliyesusia chakula alinyanyaswa na kovu za majeraha aliyo nayo zinathibitisha hayo akiwa ni mtu maarufu kijijini kwao huko Nyala.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vikosi vya usalama Darfur

Halikadhalika jina lake linatambuliwa na raia wa Sudan walio nchini Uingereza.

Chini ya sheria za Uingereza watu walioponyoka visa kama kunyanyaswa hawapaswi kuzuiliwa na afisi ya uhamiaji ingawa makundi yanayotetea haki za binadamu yanadai kua sheria hio haizingatiwi.

Watu hao waliomba waruhusiwe wageni na waungaji mkono wao kutoka Oxford walipanga ziara huru ifanywa majira ya magharibi tareh 30 May.

Licha ya mipango yote hio kila walipofika mlangoni walikataliwa kwa sababu zisizoeleweka na mara nyingine bila kutoa sababu pindi walipotambua kua ni wageni wa watu kutoka Sudan.

Hata wageni wengine ambao ziara yao haikuhusiana na hii ya wa Sudan walikataliwa bila kupewa sababu.

Wageni wa kwanza, Nazar Eltahir Mwenyekiti wa Jamii ya Wasudan huko Oxford pamoja na Tim Flatman huyu ni mwanaharakati wa haki za binadamu ambaye mara kwa mara husafiri kwenda Sudan akiunga mkono Wasudan na wahamiaji wa Sudan ya kusini walio hapa Uingereza waliambiwa kua mtu wanayemtafuta hakutarajia mgeni yeyote wala hawatambui.

Waliomba aulizwe mara nyingine na baada ya mda wakidai kua wamemuuliza walirejea na majibu yale yale. Wahudumu walidai kua wamezungumza naye kupitia mkalimani.

Wakati wakiondoka kituoni walimpigia simu akawajibu kua anawasubiri na kwamba hajapokea ujumbe wowote kuhusu kama wamefika kutimiza ziara yao.

Wageni wengine waliambiwa kua hawakupanga ziara zao mapema licha ya majina yao kua kwenye orodha ya majina yaliyoachwa juu ya meza.

Image caption Uhamiaji wakiuka sheria

Waungaji mkono wamenuwia kuendelea na juhudi za ziara yao kuwaunga mkono na vilevile wamesema watawasilisha malalamiko yao juu ya kituo hicho kwa jaribio la kuficha kisa cha kususia chakula na vilevile kuvunja sheria kwa kuwakatalia kuonana nao.

Malalamiko hayo watayafikisha kwa Waziri wa Uhamiaji, mkuu wa magereza na bodi huru inayosimamia masuala kama hayo halikadhalika mbunge wa eneo hilo.

Wakati huo huo Jamii ya Wa Sudan wanaoishi huko Carfax, Oxford kwa ushirikiano na makundi yanayotetea haki za binadamu yameandaa maandamano Ijumaa tarehe 1 Juni kuunga mkono watu hao waliosusia chakula.