Sherehe za Diamond Jubilee zaanza

Imebadilishwa: 2 Juni, 2012 - Saa 14:28 GMT

Sherehe za siku nne zinaanza Jumaosi Uingereza, kuadhimisha miaka 60 ya tangu Malkia Elizabeth kuvikwa taji - sherehe za Diamond Jubilee.

Mizinga ikipigwa Jumamosi London, kusherehekea miaka 60 ya utawala wa Malkia Elizabeth

Jumamosi, mizinga 41 ilisikika mjini London siku alipochukua umalkia rasmi.

Malkia anahudhuria mashindano ya mbio za farasi - Epsom Derby.

Na Jumapili mlolongo wa meli na mashua 1000 zitamsindikiza kwenye Mto Thames.

Karabai zaidi ya 4000 zitawashwa sehemu mbali-mbali za dunia, kusherehekea Malkia Elizabeth kutimiza miaka 60 kwenye kiti cha ufalme.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.