Rais Banda auza ndege ya rais

Rais wa Malawi, Joyce Banda, ameamua kuuza ndege ya rais pamoja na magari 60 ya fakhari.

Haki miliki ya picha AFP

Ndege hiyo ilinunuliwa kwa dola milioni-13 na rais aliyemtangulia, Bingu wa Mutharika, aliyefariki mwezi wa Aprili.

Rais Banda amenukuliwa kusema kwamba anatosheka kusafiri kwenye ndege za abiria kama watu wengine, kwa sababu ameshazowea kutembea kwa miguu na kusaidiwa na wasafiri njiani.

Fedha zitazopatikana katika mauzo ya ndege na magari hayo, zitatumiwa kuwasaidia maskini wa Malawi.

Serikali ya Uingereza, ambayo ndio mfadhili mkubwa wa koloni yake hiyo ya zamani, imepokea vema uamuzi huo kuwa ni ishara inayotia moyo.