Rais wa Somalia azuru Tanzania

Rais wa Somalia, Sharif Sheikh Ahmad, yuko nchini Tanzania kwa ziara rasmi.

Haki miliki ya picha Reuters

Waziri wa Mambo ya Wanawake wa Somalia, Bibi Mariam Aweis alisema wamekwenda Tanzania kwa mwaliko wa Rais Kikwete.

Alieleza kuwa wamezungumza juu ya uwezekano wa Tanzania kuwapatia mafunzo ya kijeshi vijana wa Somalia, na usalama kwa jumla.

Alipoulizwa kama waliomba ushirikiano juu ya tatizo la uharamia kutoka Somalia katika mwambao wa Afrika Mashariki pamoja na Tanzania, waziri huyo alisema maswala hayo yanahusiana na mafunzo ya kijeshi, ili kuwezesha Somalia kupambana na uharamia na mashambulio yanayofanywa na baadhi ya Wasomali katika nchi jirani.