Maandamano zaidi yazuka Misri

Waandamanaji katika medani ya Tahrir Haki miliki ya picha d
Image caption Waandamanaji katika medani ya Tahrir

Malefu ya raia walikesha katika medani ya Tahrir mjini Cairo, kupinga kile walichokitaja kama, kesi iliyoborongwa dhidi ya rais aliyeondolewa madarakani Hosni Mubarak.

Waandamanaji hao wameghadhabishwa kuwa Mubarak na waziri wake wa usalama wa ndani Habib el-Adli, hawakuhukumiwa kifo kuhusiana na mauaji wa waandamanaji mwaka uliopita.

Maafisa waandamizi sita wa polisi waliondolewa mashtaka ya kuhusika na mauaji hao.

Wakati huo huo, Baraza la Kijeshi linaloongoza taifa hilo, limeipa bunge la nchi hiyo masaa 48 kukamilisha shughuli ya kuteua jopo ambalo litaongoza mikakati ya marekebisho ya katiba, la sivyo baraza hilo litalazimika kutoa suluhisho bila kulishauri.

Wanasiasa wasioegemea upande wa kidini wamewashutumu wanasiasa wa Kiislamu kwa kujaribu kutawala jopo hilo.