Kamati ya katiba kuteuliwa Misri

Baraza la Kijeshi linalotawala nchini Misri Haki miliki ya picha i
Image caption Baraza la Kijeshi linalotawala nchini Misri

Ripoti zinasema kuwa mzozo uliokuwa umeibuka kuhusu jopo maalum la kuandika katiba mpya nchini Misri hatimaye imetatuliwa.

Shirika la habari la serikali la MENA limeripoti kuwa baraza la kijeshi linalotawala nchini humo na vyama vya kisiasa vinavyoakilishwa katika bunge la nchi hiyo wameafikiana kuhusu jinsi ya kuteua wajumbe watakaohudumu katika jopo hilo la kuandika katiba.

Ripoti hiyo imesema bunge la nchi hiyo litakutana wiki ijayo kuteuawa wanachama watakaohudumu katika kamati hiyo.

Mpango huo ulikuwa umekwama kutokana na mzozo kati ya wanasiasa wa Kiislamu na wale wasioegemea upande wowote kidini ambao walidai kuwa makundi ya kidini yalikuwa yakijaribu kutawala jopo hilo.