Wakili wa ICC akamatwa Libya

Wakili wa Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, amekamatwa nchini Libya, akishutumiwa kuwa alimpa Seif al-Islam - mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya, Kanali Gaddafi - nyaraka za hatari.

Haki miliki ya picha AFP Photo

Wakili huyo, Melinda Taylor, amezuwiliwa katika mji wa Zintan, magharibi mwa Libya, ambako alikwenda kumhoji Seif al-Islam kwa ruhusa ya wakuu wa Libya.

Seif al-Islam anakabili mashtaka na ICC na wakuu wa Libya, kwa yale aliyofanya kuzima upinzani uliopelekea Kanali Gaddafi kupinduliwa.