Wajumbe wa ICC watembelea wenzao Libya

Ajami Libya Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ajami Libya

Wajumbe kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, wamewatembelea wenzao wanaoshikiliwa katika mji mlima wa Zintan nchini Libya , Afisa mwandamizi amesema.

Ahmed al-Jehani, mjumbe wa ICC nchini Libya amesema hatimaye ujumbe huo umeruhusiwa kuingia katika mji huo baada ya kucheleweshwa hapo awali.

Wafanyakazi wanne wa ICC walishikiliwa wakati walipokuwa wamekwenda Zintan kukutana Saif al-Islam Gaddafi, mtoto wa marehemu Muamar Gaddaf kiongozi zamani wa Libya.

Mtu mmoja kati yao alituhumiwa kujaribu kumpa nyaraka kutoka kwa Ally mshirika wake wa zamani.

Mahakama hiyo ya The Hague , serikali ya Australia na makundi ya haki za binadamu wote walikuwa wakishinikiza wafanyakazi hao waachiliwe haraka.

Mahakakama ya ICC imesema kuwaweka kizuizini wafanyakazi hao ni kinyume cha sheria kwa kuwa wana kinga ya kutofunguliwa mashitaka.

Lakini Tripoli inasema watuhumiwa wamehatarisha usalama wa taifa na watashikiliwa kwa muda wa siku 45 wakati wakichunguzwa.

Wanamgambo wa Zintan walimteka Saif al-Islam Novemba mwaka jana na tangu wakati huo wamekuwa wakikataa kumkabidhi kwa serikali ya Libya.