Tikiti za Olimpiki zauzwa kimagendo

Kamati kuu ya Olimpiki inachunguza tuhuma kwamba baadhi ya wawakilishi wa Olimpiki wako tayari kuuza maelfu ya tikiti ya michezo ya London, kwa magendo.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Kamati ya Olimpiki, IOC, imesema inazipa uzito tuhuma hizo zilizotolewa kwenye gazeti moja la Uingereza, Sunday Times.

Gazeti hilo limesema maafisa na mawakala, kutoka nchi zaidi ya 50, walikuwa tayari kuwauzia tikiti waandishi wa habari waliojifanya kuwa wanawakilisha walanguzi.

Tikiti za michezo maarufu zilipatikana kimagendo kwa bei mara kumi zaidi ya bei rasmi.

Waandalizi wa michezo hiyo mjini London walisema, kuwa hakuna tikiti yoyote iliyonunuliwa kimagendo na waandishi hao wa habari, ambayo imetokana na wao.