Ethiopia yahamisha watu "kwa nguvu"

Imebadilishwa: 18 Juni, 2012 - Saa 12:15 GMT

Serikali ya Ethiopia imelaumiwa kwa kuwahamisha kwa nguvu maelfu ya watu kutoka mashamba yao ili kuacha nafasi kwa upanzi wa miwa

Baadhi ya watu wanaohamishwa toka bonde la Omo

Kwa muujibu wa shirika la Human Rights Watch lililona makao yake mjini New York, uhamishaji huo wa watu unafanyika katika bonde la Omo.

Bonde hilo ambalo limeorodheshwa kama sehemu ya kuhifadhiwa duniani ,pia ndipo mahali bwawa kubwa limepangwa kujengwa. Ujenzi wa bwawa hilo tayari limezua utata.

Lakini serikali ya Ethiopia imekanusha madai hayo ya kuwahamisha watu kwa nguvu huku ikijitetea kwamba mradi huo utazalisha nafasi zaidi za kazi.

Nalo shirika la Human Rights Watch limesema kuwa maafisa wa usalama wanawahamisha watu kwa nguvu kutoka eneo hilo na kuwalazimisha kurudi katika ardhi zao za kiasili.

Katika ripoti yao, shirika hilo limesema wakati waliopkuwa wakizuru eneo hilo mwezi wa June 2011,walishuhudia makundi ya kijeshi yakiwahangaisha na kutisha watu ili wahame na kutoa nafasi kwa upanzi wa miwa. Katika harakati hizo wanajeshi wanadaiwa walikuwa wakiiba na kuwauwa mifugo.

Hata hivyo serikali ya Ethiopia imekanusha madai hayo.

Msemaji wa serikali Bwana Bereket Simon amesema palipokuwa na haja ya kuwahamisha watu , wahusika sote walishauriwa na pia kushirikishwa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.