Ulaya:mdororo haukuanzia kwetu

Haki miliki ya picha afp
Image caption Viongozi wa G20

Viongozi wa Mataifa Tajiri Kabisa Duniani wanakutana kwa siku ya pili leo kwa mazungumzo nchini Mexuico, huku wasiwasi ukiendelea kuzonga mataifa ya Bara hilo kuhusiana na madeni makubwa wanayokabiliana nayo.

Taarifa iliyotolewa kuhusu mkutano huo, pendekezo linalotolewa ni kwamba viongozi wataahidi wa ukanda wa bara Ulaya wafanye kila juhudi kutatua mzozo wa madeni katika nchi zinazotumia Sarafu ya Euro.

Suala hili limegubika mkutano wa mataifa ya G20 unaofanyika nchini Mexico, ambako mwandishi mmoja wa habari alisema kuwa viongozi wa ulaya hawakuwa na hadhi.

Mwandishi huyo alikaripiwa sana na Mkuu wa tume ya Muungano wa Ulaya Jose Manuel Barroso alipouulizwa kwa nini nchi za Amerika ya kaskazini zisaidie kutatua mdororo wa sarafu ya Euro. Bwana Barroso aisema Matatizo hayakuanzia Ulaya.

"Msukosuko huu haukuanzia Ulaya, Msukusuko ameanzia Marekani ya Kaskazini na Mashirika yetu ya kifedha yaliambukizwa, na sijui nitaelezaje? Kwani kunasheria za masoko ya kifedha hazikutimizwa."

Lakini hakuna haja ya kuwalaumu washiriki wetu, tunachosema ni tushirikiane kwa pamoja wakati tunapokuwa na matatizo ya kidunia. Kama tatizo tulilo nalo leo." alisema bwana Barroso

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jose Manuel Barroso

Aidha bwana Barroso amesema muungano wa Ulayan sio wa kulaumiwa pekee kwa Mdororo wa Uchumi Duniani, na kwamba Viongozi wa Ulaya hawakwenda Mexico ili wakakaripiwe.nuel Barroso

"Sisi siyo kama hatujali. Sisi tupo wazi katika ugumu wa hali yetu, ningependa washiriki wetu nao wawe wazi. Na hatukuja hapa kujifunza kutoka kwa mtu." aliongeza Barroso

Wakati huohuo, China pamoja na nchi zingine chumi ibushi zimetoa mabilioni ya dola kwa shirika la fedha duniani IMF, pesa zitakazokwenda katika mfuko wa shirika hilo wa dharura wa shirika hilo.

China imetoa dola bilioni arobaini na tatu huku nchi zingine kama India, Brazil, Afrika Kusini na Urusi nazo zikitoa dola bilioni kumi kila mmoja, lakini hatimaye lengo pesa hizo ni kusaidia nchi za ukanda wa Euro zinazokabiliwa na matatizo ya kiuchumi.

Hizi uchumi ibushi zinakabiliwa na changamoto zako kiuchumi, ingawa zimejitolea kusaidia bara ulaya katika matatizo yake. Je ni kujitolea tu ana China na wenzake wanalenga nini katika hatua zao?