Mazungumzo ya amani ya Sudan yaendelea

Mazungumzo yanaendelea mjini Addis Ababa, Ethiopia, kujaribu kumaliza mzozo wa mpaka baina ya Sudan na Sudan Kusini, ambao katika miezi ya karibuni ulitishia kuzusha vita kamili.

Haki miliki ya picha INTERNET

Wadadisi wanasema tatizo kubwa kwenye mazungumzo hayo ni wapi kuweka mstari wa mpaka utaotenganisha nchi mbili hizo, na kuweka eneo la amani la mpakani.

Ingawa wapatanishi wamezihakikishia pande zote mbili, kwamba mstari huo utakuwa wa muda tu, hata hivo Sudan na Sudan Kusini hawaamini hayo - wanaona mwishowe utakuwa mpaka wa kudumu baina yao.

Mazungumzo ya upatanishi yanaongozwa na rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, na yanaungwa mkono na nchi jirani, pamoja na wawakilishi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.