Waziri wa Libya arejeshwa nyumbani

Imebadilishwa: 24 Juni, 2012 - Saa 14:20 GMT

Tunisia imemrejesha nyumbani waziri mkuu wa zamani wa Libya, El-Baghdadi Al-Mahmoudi.

Waziri mkuu wa zamani wa Libya, Al-Mahmoudi

Bwana Al-Mahmoudi alikuwa waziri mkuu kwa miaka mitano katika serikali ya Muammur Gaddafi, kabla ya kukimbilia Tunisia mwezi wa Agosti, wapiganaji wa Libya walipouteka mji mkuu, Tripoli.

Tangu wakati huo amekuwa gerezani mjini Tunis, huku wakuu wepya wa Libya wamekuwa wakiomba mara kadha kwamba arudishwe nyumbani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.