Wafanyikazi wa kigeni watekwa nyara Kenya

Image caption Ramani ikionyesha Dadaab

Wafanyikazi wanne wa misaada na raia mmoja wa kenya wametekwa nyara katika kambi ya wakimbizi wa Kisomali kaskazini mwa Kenya. Rubaa zinasema msafara wa wafanyikazi kutoka shirika la kuwahudumia wakimbizi la Norway ulishambuliwa na watu waliokua na silaha katika kambi ya Dadaab.

Polisi wamesema dereva wa gali lililowabeba wafanyikazi hao aliuawa kwenye makabiliano. Wafanyikazi kadhaa wa misaada walitekwa nyara katika kambi hiyo ya Dadaab mwaka jana hatua iliyolazimisha mashirika mengi yamesimamisha shuguhuli zao .

Maafisa wa shirika la wakimbizi mjini Oslo wamepokea taarifa kuhusu tukio hilo lakini hawajathibitisha kuhusu usalama wa wafanyikazi wao.Somalia imekuwa bila utawala thabiti tangu mwaka 1991 kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wapiganaji wa Kiisilamu wa Al Shabaab ambao wanashirikiana na mtandao wa Al-Qaeda wanadhibiti maeneo mengi ya nchi.Mwaka jana kundi hilo lililaumiwa kwa utekaji nyara nchini Kenya hatua iliyopelekea majeshi ya Kenya kuingia Somalia ili kukabiliana na wapiganaji wa Al Shabaab.