Annan aonya ufumbuzi wahitajika Syria

Mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, amewaonya mawaziri wa mashauri ya nchi za nje wanaokutana kujadili Syria, kwamba kushindwa kufikia makubaliano kuhusu namna ya kumaliza ghasia katika nchi hiyo, kutazusha msukosuko wa kimataifa.

Haki miliki ya picha Reuters

Bwana Annan aliuambia mkutano unaofanywa mjini Geneva kwamba mataifa makuu yatabeba sehemu ya dhamana ya vifo zaidi vitavyotokea Syria, iwapo watashindwa kufikia makubaliano.

Urusi na mataifa ya magharibi bado hayajakubaliana kama rais wa Syria anafaa kubaki kwenye uongozi.

Urusi inakataa chagizo kuwa Rais Assad anafaa kulazimishwa kuondoka madarakani.