Makaburi ya kale yavunjwa Timbuktu

Nchini Mali, wakaazi wa mji wa Timbuktu - mji wa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa - wanasema wapiganaji wa Kiislamu wamelivunja kaburi la shekhe mkubwa wa karne ya 15, Sidi Mahmoud.

Haki miliki ya picha AFP

Wanasema makaburi mengine ya kale yanashambuliwa.

Msemaji wa kundi la Kiislamu la Ansar Dine - ambalo linadhibiti eneo kubwa la kaskazini mwa Mali - alisema makaburi yote 16 ya kale ndani ya mji huo yatavunjwa.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia utamaduni, limesema mashambulio hayo yanasikitisha, na limetoa wito kwa wapiganaji hao kuacha kufanya hivo.

Ansar Dine inaamini kuwa kuabudu mashekhe wakubwa wa kale kunakwenda kinyume na Uislamu.

Wapiganaji wa Kiislamu na wa kabila la Tuareg awali mwaka huu waliliteka eneo la kaskazini mwa Mali, baada ya mapinduzi ya serikali kuu