Senegal yachagua wabunge

Wananchi wa Senegal wanapiga kura kuchagua wabunge 150.

Haki miliki ya picha AFP

Huu ndio uchaguzi wa kwanza tangu Bwana Macky Sall kuchaguliwa kuwa rais mwezi wa March.

Viongozi wote wa siasa waliomuunga mkono Bwana Macky Sall aliposimama dhidi ya Rais Abdoulaye Wade, ambaye akigombea muhula wa tatu wa uongozi awali mwaka huu, bado wameungana kuhakikisha kuwa serikali ya mseto ina viti vya kutosha bungeni.

Katika uchaguzi huu piya, kwa mara ya kwanza, idadi ya wagombea uchaguzi imegawiwa sawasawa baina ya wanawake na wanaume.

Serikali ya mseto ina kazi kubwa ya kupambana na matatizo muhimu, kama ukame na kupanda kwa bei za bidhaa.

Piya imeanzisha kampeni ya kupiga vita ulaji rushwa, huku mawaziri kadha wa zamani wanachunguzwa jinsi walivopata utajiri wao.

Serikali ya Bwana Sall imeahidi kuokoa mali yoyote ya taifa iliyoibiwa.

'