Daktari wa Ikulu akamatwa Venezuela

Rais wa Venezuela Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Venezuela

Daktari mmoja ambaye anafanya kazi katika ikulu ya rais nchini Venezuela, amekamatwa baada ya kushukiwa kuwa anafichua siri za serikali.

Waendesha mashtaka nchini humo wanasema Daktari Ana Maria Abreu, alifichua siri za kijeshi na kisiasa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Hata hivyo taarifa hiyo rasmi haikumtaja rais wa nchi hiyo Hugo Chavez, ambaye anaendelea kupokea matibabu ya ugonjwa wa saratani ambao hautatajwa.

Daktari Abreu, sio daktari wa kibinafsi wa rais Chavez, ambaye mwezi Oktoba mwaka huu anawania muhula mwingine kuwa rais wa nchi hiyo.