Afghanistan yataraji ahadi ya misaada

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Japani, Koichiro Gemba, anasema nchi yake itaahidi dola bilioni tatu zaidi, kuisaidia Afghanistan.

Haki miliki ya picha AFP

Alisema hayo kabla ya mkutano mkubwa wa wafadhili wa Afghanistan ambao utafanywa mjini Tokyo Jumalipi.

Bwana Gemba alisema jumla ya dola bilioni 16, zitaahidiwa kwenye mkutano huo, kuisaidia Afghanistan baada ya NATO kuondosha majeshi yake.

Hapo awali, Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Marekani, Hillary Clinton, alitangaza kuwa Marekani inaiona Afghanistan kuwa rafiki mkubwa na itashirikishwa katika ushirikiano wa kijeshi siku za mbele