Vita vya Syria vyarukia mpaka wa Libnan

Taarifa kutoka kaskazini mwa Libnan zinaeleza kuwa mizinga iliyofyatuliwa Syria, imepiga kijiji nchini humo na kuuwa watu watatu.

Haki miliki ya picha Reuters

Wakaazi wa kijiji walisema walisikia miripuko, katika eneo la Wadi Khaled, karibu na mpaka na Syria.

Wasyria kadha wamejificha huko baada ya kukimbia fujo za nchini mwao.

Katika siku za karibuni, kumetokea mapambano ya risasi na makombora baina ya watu wenye silaha walioko upande wa mpaka wa Libnan, na wanajeshi wa Syria, upande wa pili wa mpaka.