Vita vya Syria vyarukia mpaka wa Libnan

Imebadilishwa: 7 Julai, 2012 - Saa 14:23 GMT

Taarifa kutoka kaskazini mwa Libnan zinaeleza kuwa mizinga iliyofyatuliwa Syria, imepiga kijiji nchini humo na kuuwa watu watatu.

KIfaru cha Syria kwenye mpaka na Libnan, karibu na Wadi Khaled

Wakaazi wa kijiji walisema walisikia miripuko, katika eneo la Wadi Khaled, karibu na mpaka na Syria.

Wasyria kadha wamejificha huko baada ya kukimbia fujo za nchini mwao.

Katika siku za karibuni, kumetokea mapambano ya risasi na makombora baina ya watu wenye silaha walioko upande wa mpaka wa Libnan, na wanajeshi wa Syria, upande wa pili wa mpaka.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.