Wananchi wa Libya wachagua bunge

Wananchi wa Libyan wanapiga kura katika uchaguzi wao wa mwanzo wa taifa kwa karibu nusu karne.

Haki miliki ya picha Reuters

Wanasiasa zaidi ya 3000 wanagombea viti katika bunge jipya, ambalo litachukua nafasi ya Halmashauri ya Mpito ya Taifa, iliyoundwa baada ya Muammar Gaddafi kuondolewa madarakani miezi tisa iliyopita.

Bunge litateua serikali ya muda na kutayarisha katiba mpya.

Uchaguzi unafanywa wakati machafuko yanazidi mashariki mwa Libya, ambako baadhi ya makundi yanalalamika kuwa hayatawakilishwa sawa-sawa.

Ijumaa, ndege iliyobeba karatasi za kura ilishambuliwa karibu na mji wa Benghazi, na afisa mmoja wa uchaguzi aliuwawa.