Mkutano kuhusu Mali waanza

Viongozi wa Afrika Magharibi wanakutana Burkina Faso kuzungumzia msukosuko wa Mali.

Haki miliki ya picha

Jumuia ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS inafikiria kuingilia kati kijeshi, baada ya kundi la Kiislamu na wapiganaji wa kabila la Tuareg kuliteka eneo la kaskazini, kwa kutumia fursa ya udhaifu wa serikali kuu wakati wa mapinduzi ya Mali.

Rais Blaise Campaore wa Burkina Faso, alisema lengo la mkutano ni kujadili kile alichoelezea kuwa tishio la kigaidi kaskazini mwa Mali, na kutafuta ufumbuzi katika msukosuko wa siasa nchini Mali.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa bado halijakubali kuingilia kati kijeshi nchini Mali.