Bunge Misri lakaidi na kukutana

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Spika Saad al-Katatni akihutubia wafuasi

Bunge la Misri limekutana kwa muda mfupi licha ya amri ya baraza kuu la kijeshi kulivunja.

Rais mpya wa nchi hiyo Mohammed Mursi, aliagiza bunge hilo kukaidi amri ya kulivunja na badala yake waanze vikao.

Mapema,baraza hilo lilitoa taarifa likisema amri ya kuvunja bunge lazima liheshimiwe. Jeshi lilifunga bunge wnezi uliopita kufuatia uamuzi wa mahakama ya juu zaidi nchini Msiri.

Muingilio huu unachukuliwa na wengi kwamba baraza la kijeshi linamuonya rais mpya Mohammed Mursi ambaye aliapishwa wiki iliyopita.

Huu ndio huenda ikawa mwanzo wa mgogoro kati ya rais huyo mpya na jeshi la nchi hiyo.

Spika wa bung Saad al-Katatni amesema kwamba hauta yao ya kukutana sio kinyume na uamuzi wa mahakama bali wanatafuta njia ya kuheshimu mahakama hiyo na kutekeleza agizo lake.

Wabunge waliunga mkono pendekezo la spika kwamba bunge litafuta ushauri kutoka kwa mahakama ya rufaa kuhusu jinsi ya kutekeleza agizo la mahakama ya juu zaidi nchini humo.

Baada ya hapo akaahirisha vikao.