AU yasema Mali ni changamoto kubwa

Mkuu wa Baraza la Umoja wa Afrika, AU, anasema mzozo wa Mali ni moja kati ya changamoto kubwa inayokabili bara hilo.

Haki miliki ya picha AFP Getty Images

Jean Ping alisema hayo mbele ya viongozi wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, rais wa Ivory Coast, Alassane Ouatarra, aliuambia mkutano huo kwamba eneo la kaskazini la Mali limekuwa hifadhi ya makundi ya magaidi, na viongozi wenzake walikubali kwamba eneo la kaskazini mwa Mali lazima lifanywe salama tena - eneo ambalo lilitekwa na wapiganaji wa Kiislamu na wa kabila la Taureg baada ya jeshi kupindua serikali kuu iliyochaguliwa.

Bwana Ping piya alisema hakujapatikana mafanikio makubwa katika kutatua mzozo baina ya Sudan na Sudan Kusini.

Kikao hicho cha kamati ya kushughulikia mizozo, kinafanywa kabla ya mkutano wa kilele wa AU utaofanywa mjini humo, Addis Ababa.