Tantawi atetea jeshi kulinda nchi

Mkuu wa baraza la jeshi la Misri lenye nguvu, inaonesha anazidisha mvutano katika mashindano yake na chama cha Muslim Brotherhood.

Haki miliki ya picha AP

Akizungumza kwenye hafla ya jeshi, Field Marshall Hussein Tantawi, alisema kwamba jeshi halitaruhusu kundi fulani kulizuwia jeshi kutekeleza kazi yake ya kulinda watu wa Misri.

Maneno yake yanaonekana kulenga chama cha Muslim Brotherhood cha Rais Mohammed Mursi.

Bwana Tantawi alisema hayo punde baada ya kukutana na Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Marekani, Hillary Clinton, ambaye alilisisitiza kuwa kipindi cha mpito cha Misri kielekeze nchi kwenye uongozi wa kiraia.