Madaraka ya serikali yameguka Syria

Moja kati ya makundi ya upinzani ya Syria, Muslim Brotherhood, linasema madaraka ya serikali yanameguka katika sehemu nyingi za nchi, na limetoa wito watu wawe na nidhamu na uvumilivu.

Limesema kila mtu anawajibika kusaidia kuendeleza usalama wa raia na haki zao za kimsingi.

Wanaharakati wa upinzani wanasema zaidi ya watu mia mbili wameuwawa katika mapigano ya Ijumaa.

Majeshi ya serikali yanasema kuwa yametimua makundi ya wapiganaji mjini Damascus.

Mapigano piya yametokea katika mji wa Aleppo.