Ulaya kuiondolea Zimbabwe vikwazo

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rais Robert Mugabe bado amewekewa vikwazo

Umoja wa nchi za Ulaya itaondoa vikwazo dhidi ya Zimbabwe mara tu nchi hiyo itakapoanda kura ya maoni iliyo huru na ya wazi kuhusu katiba yake mpya.

Mawaziri wa mambo ya nje wa umoja huo wamesema kuwa katiba nzuri na inayokubalika na raia wengi ni hatua muhimu kwa nchi hiyo kuandaa uchaguzi huru na wa haki.

Katika taarifa yao mawaziri hayo wamewaondolea vikwazo zaidi ya wapambe 100 wa rais Robert Mugabe.

Viongozi zaidi ya 100 wa Zimbabwe akiwemo Rais Mugabe mwenyewe waliwekewa vikwazo tangu mwaka 2002 vikiwemo kupigwa marufuku kusafiri nchi za Ulaya.

Lakini William Hague,waziri wa Maswala ya njee wa Uingereza amesema kuwa Rais Mugabe hakuondolewa vikwazo.

Vikwazo hivyo vilivyoweka zaidi ya muongo mmjoja uliopita yalifuatia madai ya Zimbabwe kukiuka haki za kibinadamu ikiwemo kuwa dhulumu na kuwanyanyasa upinzani.

Rais Mugabe na mpinzani wake Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai, wamekuwa katika serikali ya ugavi wa madaraka kufuatia utata uliokumba uchaguzi wa Zimbabwe wa mwaka 2008.

Uchaguzi mwengine unatarajiwa kuandaliwa mwaka ujao wa 2014 baada nchi hiyo ya kusini mwa Afrika kupata katiba mpya.

Kwa muda mrefu wapambe wa Rais Mugabe wamekuwa wakitaka vikwazo hivyo viongolewe bila masharti yeyote wakidai kuwa vinaathiri uchumi wa Zimbabwe.

Nchi hizo za Ulaya zilisema zinafurahishwa sana na hatua ya nchi za SADC kutaka kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Zimbabwe.