Mapigano yachacha Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mapigano Syria

Mapigano makali yameendelea kati ya wanajeshi watiifu kwa serikali ya Syria na waasi katika miji ya Damascus na Aleppo.

Rubaa za karibuni zikisema ndege za kijeshi zimembulia kwa mabomu mji wa Aleppo.

Huku haya yakiarifiwa mashirika ya misaada yamesema kwamba idadi ya watu wanaohijaji msaada wa dharura inazidi kuongezeka.

Waziri Mkuu wa Iraq ,Nuri al-Maliki amearisha wanajeshi wanaolinda mpaka wake kuwakubalia wakimbizi wanaotoka Syria kuingia eneo la upana wa kilomita 600.

Mpaka wa Rabiya umeendelea kufungwa baada ya majeshi kuudhibiti tena siku chache baada ya kutwaaliwa na waasi. Athel al-Nujaifi ni gavana wa eneo hilo.

Haki miliki ya picha x
Image caption Wananchi wa Syria

Wanaharakati wanaopigana dhidi ya serikali wanasema kuwa kumetokea vurugu katika magereza katika miji ya Aleppo -- ambao ndio mkubwa kwa upili nchini Syria na Homs. Wanaharakati walielezea kuwa takriban watu tisa waliuawa katika gereza la Aleppo.

Wanahofia kuwa watu wengi zaidi huenda wamejeruhiwa huku wanajeshi wa serikali wakijiandaa kushambulia magereza katika miji hiyo miwili.

Wakati huohuo, televisheni imekuwa ikionyesha picha za machafuko kusini mwa Damascus na maiti za watu walioitwa kama magaidi waliouawa katika makabiliano huko.

Ilisema kuwa majeshi ya serikali yamewefanikiwa kutwaa sehemu nyingi za mji mkuu ambako mapambano makali yalishuhudiwa huko wiki jana.

Image caption Damascus

Susan Ahmad, ni msemaji wa baraza kuu la mapinduzi mjini Damascus, alisema ni vigumu kwa wenyeji kutoka nje ya nyumba zao kwa sababu ya mapigano makali.

Rais wa Marekani, Barack Obama ameonya kuwa rais Bashar al-Assad atakuwa anafanya kosa kubwa sana ikiwa atatumia silaha za keimikali ambao sasa Syria imeitikiwa kumiliki. Obama ameyasema hayo mjini Nevada na kuongeza kuwa rais Assad atawajibihsw avikali ikiwa atatumia silaha hizo dhidi ya raia wake.

Awali msemaji wa wizara ya mambo ya nje nchini humo alisema kuwa kamwe Syria haiwezi kutumia zana za sumu dhidi ya watu wake, lakini itaweza kuzitumia tu ikiwa watashambuliwa na nchi yoyote ya kigeni. Kiongozi wa baraza la kitaifa la upinzani nchini humo Abdelbasset Sieda, alisema kuwa syria tayari imeonekena kutokuwa na hofu ya kutumia silaha hizo.