Syria yapeleka majeshi Aleppo

Maelfu ya wanajeshi wa Serikali imeripotiwa kwamba wanaelekea katika mji wa Aleppo wa pili kwa ukubwa nchini humo.

Hii inaonekana kama sehemu ya jitihada ya kuyatwaa maeneo ya mji huo ambayo kwa sasa yanashikiliwa na waasi.

Mwanajeshi mmoja wa Free Syria Army amesema kuwa wameshambuliwa majeshi ya serikali hasa katika eneo la Jabal al-Zawiya area.

katika siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa mapigano makali katika mji wa Aleppo.

Serikali imekuwa ikielekeza helikopta , ndege za kivita na maelfu ya wanajeshi ili kulirudisha nyuma jeshi la upinzani.

Lakini katika mji wa Damascus, majeshi ya serikali yanaonekana kuyazidi nguvu jeshi la upinzani.

Wapiganaji wa upinzani wa Free Syrian Army wamesema maelfu ya askari wakiwa na vifaru na magari ya deraya walmekuwa wakiondoka jimbo la Idlib karibu na mpaka wa Uturuki ili kuelekea Aleppo.

Vikundi vya upinzani vinasema maeneo ya vitongoji vya mji wa Aleppo na mji mkuu Damascus yameshambuliwa kwa silaha nzito wakati serikali ikijaribu kurejesha udhibiti wake katika maeneo hayo.