Mshambuliaji wa Colorado alipanga mauaji

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mshukiwa James Holmes

Mtu anayeshukiwa kuwaua watu kumi na mbili kwa kuwapiga risasi kwenye ukumbi wa sinema mjini Denver Colorado wiki jana, alituma daftari yenye maelezo ya mauaji makubwa aliyonuia kufanya kwa mtaalamu wa matibabu ya magonjwa ya akili chuoni mwake.

Taarifa hizi ni kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani.

Daftari hiyo ilikuwa na picha za michoro ya watu na maelezo yake kuhusu mashambulizi yatakayojiri.

Chuo kikuu cha Colorado, Denver, kimethibitisha kuwahi kupokea mzigo ambao hawakujua ulikotoka ingawa waliweza kuukabidhi kwa polisi.

James Holmes,mwenye umri wa miaka 24, amekamatwa na polisi kuhusiana na mauaji hayo katika ukumbi wa sinema mjini Aurora.

Taarifa hizi zimetolewa wakati mazishi ya Gordon Cowden, mmoja wa watu kumi na wawili waliouawa yakifanyika. Wanawe Gordon Cowden mwenye umri wa miaka 51 walikuwa pamoja naye ingawa waliponea.

Maelezo

Kituo cha televisheni cha Fox News, kikitaja afisaa wa polisi mwenye kuwapa habari hizi , kilikuwa cha kwanza kufichua taariza zenyewe kuhusu daftari hiyo.

Kulingana na kituo hicho, daftari hiyo ilikuwa na maelezo kamili kuhusu namna James alivyokuwa anapanga mauaji yake , picha za kile alichokuwa ananua kufanya na maelezo ya kina kuhusu njama yake.

Vyombo vingine vya habari vilinukuu duru kadhaa zikisema kuwa Holmes, aliyekuwa anapanga kuacha masomo alituma mzigo fuochuoni mwake.

Lakini wakuu wa chuo cha Denver walionekana kutofautiana na taariza za vyombo vha hyabari,kuwa mzigo huo ulutumwa kabla ya mauaji yake na kuwa ulisalia kufungwa kwa siku kadhaa.

Maafisa kwenye kitivo cha mafunzo ya utabibu cha Anschutz walisema walipokea mzigo huo ingawa waliukabidhi kwa polisi mara moja. Polisi hata hivyo walikataa kuzungumzia taarifa hiyo siku moja baada ya jaji anayesikiliza kesi ya mshukiwa kuonya maafisa wakuu kuwa maakini kuhusu taarifa wanazotoa kuhusiana na kesi hiyo.