Zanzibar yapiga marufuku meli tatu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Uokoaji baada ya Ferry ya MV Skagit kuzama

Serikali ya Zanzibar imefuta usajili wa meli tatu ikiwa ni mojawapo ya jitihada ya serikali hiyo kupunguza visa vya ajali za baharini.

Serikali pia imeliagiza halmashauri ya kusimamia usafiri ,Surface and Marine Regulatory Authority(SUMATRA),kuongeza utenda kazi wake hadi Zanzibar

Hatua hii inakuja wiki moja baada ya meli ya MV Skagit kuzama baharini wakati ikielekea zanzibar.

Miongoni mwa meli hizo zilizoharamishwa ni MV Kalama ambayo pia inamilikiwa na wenye MV Skagit.

Katika ajali hiyo watu zaidi ya 150 walikufa maji.

Hii nikauja siku moja tu baada ya Serikali ya Tanzania kuagiza SUMATRA kufanya kazi yake ipaswavyo.

Katika agizo lake Waziri katika ofisi ya Makamu wa Rais Mohammed Aboud amesema SUMATRA lazima ikague meli zote za Zanzibar kuangalia kama zinastahili kuwa baharini au la.