Mbeki asema mapatano yamepatikana Sudan

Mpatanishi wa Umoja wa Afrika, Thabo Mbeki, ametangaza mapatano baina ya Sudan na Sdudan Kusini kuhusu malipo ya mapato ya mafuta baada ya mzozo wa miezi kadhaa, ambao ulikaribia kuingiza mataifa hayo mawili vitani.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Bwana Mbeki aliwaambia waandishi wa habari katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, kwamba maswala yote yaliyokuwa yamebaki, sasa yametatuliwa, lakini hakutoa maelezo zaidi.

Sudan na jirani yake hawakusema kitu hadi sasa.

Sudan Kusini ilisitisha usafirishaji wa mafuta kupitia Sudan mwezi wa Januari, kufuatia mzozo kuhusu ada iliyokuwa ikitozwa na serikali ya Khartoum.