Vita vya Aleppo vyazidi kuwa vikali

Duru za kijeshi zinasema kuwa wanajeshi 20,000 wa Syria sasa wako katika eneo la mji wa Aleppo, ambako jeshi linapigana kuwatoa wapiganaji mjini humo.

Haki miliki ya picha Reuters

Ndege za kijeshi, helokpta zenye bunduki kubwa na mizinga inashambulia maeneo ya wapiganaji.

Lakini mwandishi wa BBC anasema wapiganaji wameongezeka mjini Aleppo, na wamejizatiti sawa-sawa.

Katika mji mkuu, Damascus, jeshi lilisema limelikomboa eneo la mwisho muhimu kwa wapiganaji.