Ugiriki haitaki wahamiaji

Polisi wa Ugiriki wamewakamata watu karibu 5,000, kwenye operesheni dhidi ya wahamiaji haramu, huku kukiwa na wasi-wasi kuwa wakimbizi kutoka Mashariki ya Kati, wanaweza kutaka kuingia kwa sababu ya vita vya Syria.

Haki miliki ya picha Reuters

Watu zaidi ya 1,000 wamekamatwa hadi sasa, na wengine zaidi wanatarajiwa kuzuwiliwa.

Wahamiaji wasiokuwa na nyaraka zinazofaa watarejeshwa makwao.

Zaidi ya 80% ya wahamiaji wanaoingai Umoja wa Ulaya, wanapitia Ugiriki.

Na baadhi ya wanasiasa wameitaka serikali ichukue msimamo mkali kuhusu wahamiaji haramu, wakati Ugiriki inapita kwenye msuko-suko mkubwa kabisa wa kiuchumi kwa miongo kadha.