Ugiriki haitaki wahamiaji

Imebadilishwa: 5 Agosti, 2012 - Saa 17:14 GMT

Polisi wa Ugiriki wamewakamata watu karibu 5,000, kwenye operesheni dhidi ya wahamiaji haramu, huku kukiwa na wasi-wasi kuwa wakimbizi kutoka Mashariki ya Kati, wanaweza kutaka kuingia kwa sababu ya vita vya Syria.

Polisi wa mpakani wa Ugiriki wakifanya doria karibu na  mpaka wa Uturuki

Watu zaidi ya 1,000 wamekamatwa hadi sasa, na wengine zaidi wanatarajiwa kuzuwiliwa.

Wahamiaji wasiokuwa na nyaraka zinazofaa watarejeshwa makwao.

Zaidi ya 80% ya wahamiaji wanaoingai Umoja wa Ulaya, wanapitia Ugiriki.

Na baadhi ya wanasiasa wameitaka serikali ichukue msimamo mkali kuhusu wahamiaji haramu, wakati Ugiriki inapita kwenye msuko-suko mkubwa kabisa wa kiuchumi kwa miongo kadha.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.