Mo Farah ashinda dhahabu Olympiki

Mo Farah mkimbiaji mashuhuri kutoka Uingereza ameshinda medali ya dhahabu mbio za mita 10,000 wanaume katika michezo ya London Olympics 2012.

Farah mwenye umri wa miaka 29 bingwa wa mbio za mita 5,000 alitumia dakika 27 sekunde 30 nukta 42 huku Mmarekani Galen Rupp akishika nafasi ya pili kwa kutumia dakika 27 sekunde 30 nukta 90 na kushinda medali ya fedha.

Tariku Bekele kutoka Ethiopia alinyakua medali ya shaba baada ya kutumia dakika 27 sekunde 31 nukta 43.

Ushindi wa Farah umeizuia Ethiopia kushinda mara nne mfululizo katika mbio hizo na kuzuia Kenenisa Bekele ushindi wa mara tatu mfululizo.

Miaka minne iliyopita jijini Beijing, Farah alishindwa kufuzu fainali za mbio za mita 5000 na toka wakati huo alikusudia kufanya juhudi zaidi.