Rais wa Somalia atoka kwenye mazungumzo

Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ametoka kwenye mazungumzo yanayofanywa mjini Nairobi, Kenya, yaliyolenga kutekeleza katiba ya Somalia iliyokubaliwa hivi karibuni.

Rais amesharudi Mogadishu, na amejaribu kuzimua habari kuhusu mzozo huo, lakini wadadisi wanasema lilikuwa pigo kubwa kwa mazungumzo hayo.

Wanasiasa waandamizi wa Somalia wanaendelea kuzungumza juu ya namna ya kumchagua rais mpya na spika.

Mazungumzo yanatarajiwa kumalizika ufikapo mwisho wa mwezi huu.