Ebola imedhibitiwa Uganda

Ebola Uganda Haki miliki ya picha AP

Shirika la msaada wa matibabu, MSF, limeelezea kuwa ugonjwa unaouwa kupitia virusi, Ebola, na uliozuka nchini Uganda, inaelekea umedhibitiwa.

Akizungumza na BBC, afisa mmoja wa MSF anayehusika na magonjwa yanayoenea kwa kuambikiza, Dk Paul Roddy, alisema kifo cha mwisho kilichosababishwa na Ebola kilitokea siku 11 zilizopita.

Lakini alionya kwamba iwapo kuna virusi eneo fulani ambavyo bado havikushughulikiwa, ugonjwa unaweza kujitokeza tena.

Alisema imethibitishwa kuwa vifo 19 vilitokana na ugonjwa uliotokea kwenye mji wa Kagadi.

Dk Roddy alisema inawezekana virusi hivo vilitokana na popo, ambao pengine waliwaambukiza nyani.

Nyama ya nyani huliwa na baadhi ya wawindaji.