Olimpiki ilizingatia mazingira

Imebadilishwa: 11 Agosti, 2012 - Saa 14:26 GMT
Olimpiki ya London

Michezo ya Olimpiki ya London imesifiwa kuwa imezingatia sana mazingira - kushinda michezo yote iliyopita.

Viwanja vya mwaka huu vilijengwa kwa nyenzo zilizowahi kutumika kabla.

Mwenyekiti wa tume ya Olimpiki, Shaun McCarthy, alisema London imejipatia medali ya dhahabu kwa kuheshimu mazingira.

Michezo iliyopita ililaumiwa kwa uharibifu kwa sababu ya ubadhirifu mwingi uliotokea, lakini viwanja vya Olimpiki ya London, vilijengwa kwa nyenzo ambazo asilimia 25 zilikuwa zimeshawahi kutumika kabla.

Tume hiyo ilisifu mawasiliano baina ya viwanja mbalimbali vya Olimpiki, lakini ililalamika juu ya bidhaa za Olimpiki zinazouzwa, kama kweli zinazingatia mazingira.

Na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alitangaza Jumamosi, kuwa riadha na mashindano ya riadha yatakuwa sehemu ya ratiba mpya za shule.

Hatua hiyo inachukuliwa wakati kuna mjadala kuhusu mafunzo yaliyojitokeza kupitia Olimpiki kufanyika London; na inafuatia malalamiko dhidi ya serikali, kwa kuondoa nafasi za kufanya mazoezi shuleni.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.