Mahindi yatakuwa haba Marekani

Ukame wa Marekani Haki miliki ya picha Reuters

Ukame mbaya kabisa kutokea Marekani kwa nusu karne na joto jingi, limesababisha uharibifu mkubwa zaidi wa zao la mahindi kushinda ilivotarajiwa.

Asilimia 16 ya zao limeharibika katika mwezi uliopita kupitia jua kali, kufuatana na takwimu za wizara ya kilimo.

Wizara hiyo inaonya kwamba inataraji kuwa zao la mwaka huu litapungua kwa asilimia 13; upungufu mkubwa kabisa tangu mwaka 1995.

Marekani ndio inayozalisha kwa wingi zaidi duniani mahindi na maharage ya soya.

Wataalamu wanakisia kuwa bei ya vyakula itapanda kwa zaidi ya asilimia 4.