Mursi aeleza kwanini amfuta Tantawi

Imebadilishwa: 13 Agosti, 2012 - Saa 13:07 GMT

Mursi akiwa na Tantawi na Jenerali Sami Annan

Rais wa Misri Mohammed Mursi amesema kuwa alikuwa na sababu nzuri na za kizalendo zilizomfanya kuwafuta kazi Mkuu wa Jeshi na Mkuu wa baraza kuu la Kijeshi.

Amesema sababu zake za kuwastaafisha wakuu hao wawili wakijeshi ni kwa faida ya taifa zima.

Rais Mursi alikuwa akizungumza baada ya kuwa badilisha vinara wa kijeshi Field Marshal Mohammed Hussein Tantawi, na mkuu wa jeshi Jenerali Sami Annan.

Rais huyo pia anadaiwa kutoa tangazo ambalo linampa madaraka na nguvu mpya za kiutawala.

Awali baraza ku la kijeshi nchini Msiri lilijilimbikizia madaraka na kuchukuwa madaraka yote ya urais mara tu baada ya kuanguka kwa utawala wa Hosni Mubarak.

Bwana Mursi amechukuwa hatua ya kufutilia mbali tangazo la mwezi Juni la Baraza kuu la kijeshi ambalo ilikuwa imeipa jeshi uwezo wa kibunge na kusimiamia makadirio ya fedha.

Haifahamiki Mahakama kuu ya kikatiba nchi humo itachukulia vipi hatua hiyo ya Rais Mursi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.