IBM kujenga maabara Nairobi

Imebadilishwa: 14 Agosti, 2012 - Saa 18:32 GMT
Barabara za mji wa Nairobi

Barabara za mji wa Nairobi

Kampuni ya kimataifa ya kutengeneza vifaa vya elektroniki IBM na serikali ya Kenya zimetangaza mpango wa kujenga maabara ya kisasa mjini Nairobi, katika juhudi za pamoja za kusaidia kupunguza msongamano wa magari mjini humo.

Kampuni hiyo ya Marekani tayari ina vituo 11 vya utafiti kote ulimwenguni.

Ripoti zinasema kampuni hiyo ina mipango ya kujenga vituo vingine 50 katika kipindi cha miaka mitano ijayo, na hivyo kuvutia mataifa mengine barani Afrika.

Katika kanda ya Afrika Mashariki, mji wa Nairobi umekuwa kivutio kikubwa cha uwekezaji kwa kampunu za kigeni.

Haijulikani IBM, itatumia kiasi gani cha fedha kufadhili mradi huo wa ujenzi wa mahabara.

Inakisiwa kuwa kampuni hiyo hutumia takriban dola bilioni sita nukta tano kila mwaka kwa utafiti na maendeleo.

Katibu wa wizara ya habari na utangazaji nchini Kenya, Dkt. Bitange Ndemo amesema serikali ya Kenya ina mpango wa kuchangia dola milioni mbili za Kimarekani katika kipindi cha miaka mitano, huku wote wakiwa na haki miliki sawa.

Mradi huo unadhamiria kukukuza matumizi ya teknolojia nchini Kenya katika maeneo ya umma.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na IBM, mwaka wa 2011, mji wa Nairobi unashikilia nafasi ya nne katika miji yenye msongamano mkubwa wa magari duniani.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.