Muamba astaafu rasmi

Imebadilishwa: 15 Agosti, 2012 - Saa 13:13 GMT
Fabrice Muamba

Fabrice Muamba

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Bolton, Fabrice Muamba ametangaza kuwa amestaafu kama mchezaji wa kulipwa wa soka.

Muamba, mwenye umri wa miaka 24, alizirai na kupata mshutuko wa moyo tarehe kumi na saba mwezi Machi mwaka huu wakati Bolton ilipokuwa ikichuana na Tottenham Hotspurs.

Akiongea na waandishi wa habari Muamba, alisema licha ya habari hizo kuwa za kuhuzunisha, anawashukuru mashabiki wake na wasimamizi wa klabu hiyo.

''namshukuru mungu kuwa niko hai hii leo na kwa mara nyingine nawashukuru sana madaktari wote ambao hawakufa moyo wakati nilikuwa na matatizo'' alisema Muamba.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.